Ajali iliyoua Mke na Mtoto wa Mfalme ni ya Kawaida

Jeshi la polisi limesema kuwa ajali iliyosababisha kifo cha mke wa mfalme wa nchi hiyo Ouk Phala ni ya kawaida nchini Cambodia.Iliripotiwa kuwa ajali mbaya ya barabani iliyotokea jumapili asubuhi mkoani Preah Sihanouk, kusini magharibi mwa Cambodia na kusababisha majeruhi ya mwana wa mfalme wa nchi hiyo Norodon Ranariddh na kifo cha mkewe Ouk ni “ajali ya kawaida”.

Kaimu Mkuu wa Polisi nchini humo Him Yan amemlaumu dereva wa taxi Mil Saret kwa kusababisha ajali hiyo mbaya, na kwamba dereva huyo amefunguliwa mashtaka ya uendeshaji mbaya na kusababisha kifo.

Amesema ajali hiyo imetokea kwa kuwa dereva aliendesha kwa kasi na kujaribu kupita gari nyingine, na kugongana uso kwa uso na gari ya mwana mfalme.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*