Kilichosababisha Wazazi na Wanafunzi kumng’ang’ania Mwalimu

Mwalimu mmoja wa shule ya msingi ameliliwa sana na Wanafunzi wake pamoja na Wazazi wao baada ya Mwalimu huyo kupata uhamisho.Mwalimu huyo wa shule moja ya msingi mjini Veliagram nchini India anayejulikana kama Mr. Bhagawan mwenye miaka 28 ameelezwa kuwa na mahusiano mazuri sana na Wanafunzi wake pamoja na Wazazi wao.

Taarifa zinasema kuwa mara baada tu ya Wanafunzi na Wazazi wao kugundua kuwa Mwalimu huyo amehamishwa katika shule yao walianza kupinga na kuandamana huku wakibubujikwa na machozi wakishinikiza mamlaka kubatilisha uhamisho wa Mwalimu huyo kwa kile walichodai kuwa wanampenda sana.

Kwa upande wake Mwalimu huyo ambaye amekuwepo katika shule hiyo kwa miaka minne ikiwa ndio sehemu yake ya kuwanza kufanya kazi ya ualimu alionekana akitokwa na machozi huku akisema kuwa amejitahidi kuishi vizuri sana na Wanafunzi hao na angependa kubaki katika shule hiyo.

Aidha maandamano hayo ya Wanafunzi yamesaidia uhamisho wa Mwalimu wao kusogezwa mbele kwa siku 10.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*