Aliyeandika mtandaoni ‘Spika wa Bunge anaumwa tumuombee’ kutupwa jela miaka sita

Bofya Hapa

Polisi nchini Indonesia inamshikiria kijana mmoja aliyeandika kwa utani mtandaoni akimdhihaki Spika wa Bunge nchini humo, Setya Novanto kuwa anaumwa hoi na kutaka watu wamuombee kisha kuweka picha yake akiwa kitandani akitibiwa na Batman (Popo mtu) huenda akafungwa miaka sita jela.

 

Picha rasmi iliyotolewa na Serikali ya Indonesia Novemba 1 mwaka huu.Kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Dyann Kemala Arrizqi aliandika ujumbe huo ambao ulitafsiriwa kama wa kichochezi na habari ya uongo.Huu ndio ulikuwa ujumbe wa kwanza nchini Indonesia kusambazwa na kijana huyo mwezi septemba imechukua miezi miwili kumkamata baada ya tangazo la serikali.

 

           Mwanasheria wa serikali nchini humo amesema kuwa hakuna picha iliyotolewa rasmi na serikali kumuonesha spika huyo jinsi anavyoishi hospitali, hivyo wote waliosambaza picha hiyo mi lazima wakamatwe na wchukuliwe hatua kwa makosa ya kimtandao.Tangazo kutoka serikalini lililotolewa na serikali mwezi uliopita baada ya kutangaza kuanza kuwafuatilia waliosambaza ujumbe huo.

Spika Setya Novanto amelazwa tangu tarehe 20 Oktoba mwaka huu katika hospitali ambayo haijawekwa wazi na serikali ya nchi hiyo na wala hajulikani ugonjwa anaoumwa.Setya Novanto anaandamwa na kesi za ubadhilifu wa fedha za umma zaidi ya dola milioni 200 na mpaka sasa hajajitokeza mbele ya bunge kujibu tuhuma hizo huku wabunge wa chama tawala cha Partai Demokrasi Indonesia Perjuangan (PDIP) wakionekana kumkingia kifua Spika huyo.

 

Hata hivyo Mawakili wa kujitegemea na wanaharakati nchini humo wamejitokeza kumtetea kijana huyo na tayari amejitetea kuwa alifanya hivyo kuutaarifu umma na atapandishwa kizimbani jumatatu ya wiki ijayo.Spika wa Bunge, Setya tangia mwaka 2015 amekuwa akikubwa na kesi za ufisadi na Taasisi ya kupambana na rushwa nchini humo Corruption Eradication Commission (KPK) lakini amekuwa akishinda kesi zote.Wanaharakati nchini humo wamembatiza jina la Satya mwenye nguvu anayetetewa na wabunge wa Chama tawala.

 

Wabunge wa Vyama vya Upinzani wanaoshinikiza Spika wa Bunge achukuliwe hatua akiwa huko huko hospitali wakidai kuwa wanaungana na kijana huyo na wengi wao tayari wameisambaza picha hiyo mtandaoni.Kwa mujibu wa sheria nchini humo kosa la kutoa habari za uchochezi au habari za uogo ni kifungo cha miaka 6 au faini dola elfu 25. Mpaka sasa makosa kama hayo yamewakumba wanaharakati 14 na tayari wamefungwa huku mamia wakisubiri hukumu ya kesi kama hizo.

Chanzo : Shirika la Global Voice