ANGALIA BINTI WA MIAKA 11 AJIFUNGUA SIKU YA HARUSI YAKE,NI MAJANGAZ

Bofya Hapa

Binti wa miaka 11 wa nchini Bulgaria ambaye alijifungua mtoto wa kike siku ya harusi yake huku akiwa amevaa shela lake la harusi amesema hataki tena kuendelea na shule na anataka atumie muda mwingi kucheza na mtoto wake.

Kordeza Zhelyazkova mwenye umri wa miaka 11 wa nchini Bulgaria alijifungua salama wiki iliyopita mtoto wa kike mwenye uzito wa kilo 2.4 ambaye alimpa jina la Violeta lakini alitoroka hospitali na mtoto wake usiku huo huo aliojifungua mtoto wake ili awahi kumalizia sherehe za harusi yake.

Kordeza ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa shule ya msingi, alisema kuwa alikutana na mumewe mpya mwenye umri wa miaka 19 Jeliazko Dimitrov kwenye viwanja vya michezo vya shule yake baada ya Jeliazko kumuokoa kutoka kwenye kipigo cha wahuni wa mitaani. Kordeza anadai alianza kufanya mapenzi na Jeliazko bila kutumia kondomu na anakiri alikuwa hajui kondomu ni kitu gani wakati huo.

Kordeza alipata mimba ndani ya wiki moja baada ya kuanza kufanya mapenzi na mpenzi wake huyo. Kordeza anasema alikuwa hajui kama ana mimba mpaka bibi yake alipoona mabadiliko ya maumbile yake, tumbo lake likizidi kuwa kubwa. “Nilifikiria labda nimekula burger nyingi sana ndio maana tumbo langu limekuwa kubwa”, alisema Kordeza.

Sitachezea tena madoli, ninalo doli langu jipya nalipenda sana”, Kordeza alinukuliwa na gazeti la News of The World la Uingereza akisema. “Sitarudi shule tena, nimeishakuwa mama”,alisema Kordeza. Wakati huo huo kuna uwezekano wa mumewe kutupwa jela miaka sita kwa kufanya mapenzi na msichana mwenye umri chini ya miaka 14.

Umri unaoruhusiwa kisheria kuanza mapenzi nchini Bulgaria ni miaka 14. “Ninaogopa sana… nataka nimtunze mtoto wangu na mke wangu lakini kuna uwezakano nikatupwa jela”, alisema Jeliazko. “Nimefanya makosa lakini sitaomba msamaha kwa sababu nimepata mtoto mrembo Violeta”, aliongeza Jeliazko. Mtoto Kordeza amedai hana mpango wa kuzaa mtoto mwingine tena.