ANGALIA MABIBI HARUSI WALIOENDA KUFANYA MTIHANI SHEREHE ZA HARUSI ZAO ZIKIENDELEA

Bofya Hapa

Mabinti wawili wa kutoka Nigeria ambao walikuwa mabibi harusi wameshangaza watu baada ya kwenda kufanya mitihani yao ya mwisho chuoni wakiwa na mashela yao mara tu baada ya kufunga ndoa. Inaelezwa kuwa mabinti hao wate walikuwa wanaolewa siku hiyo moja na kwa isivyo bahati, mtihani ambao ulipangwa kufanyika mwezi February uliahirishwa na kupangwa kufanyika siku ambayo mabinti hao na familia zao walipanga iwe siku ya harusi.

Iliwabidi wote wawili wafunge ndoa na kukimbia chuoni ili kufanya mtihani huo na baadaye kwenda kuendelea na sherehe ya harusi kama ilivyopangwa

Mabibi harusi hao Dorcas Atsea na Deborah Atoh walikuwa wanafunzi wa Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu cha Mji wa Benue walikuwa wanafanya mtihani wao wa mwisho wa somo la “Media Ethics and Law”.