ANGALIA MAFURIKO YASABABISHA VIFO VYA WATU TISA DAR ,NI MAJANGA

Bofya Hapa
DCIM100MEDIADJI_0037.JPG

MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita zimesababisha mafuriko aktika maeneo mbalimbali ya jiji huku watu kadhaa wakiripotiwa kufariki dunia kutokana na mvua hizo. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi, Lazaro Mambosasa amesema amepokea taarifa ya watu tisa kufariki dunia kutokana na mvua hizo huku wengine wakijeruhiwa.

Kamanda Mambosasa amesema vifo hivyo vimetokana na kuangukiwa na ukuta na wengine kusombwa na maji kutokana na mvua zilizonyesha kwa siku tatu mfululizo. Mambosasa amesema mwili mmoja uliosombwa na mafuriko umekutwa ukielea majini kuelekea eneo la Jangwani. Aidha, mamia ya wakazi wa jiji hilo wameripotiwa kupoteza makazi yao kutokana na maafa hayo huku wengine wakipoteza mali zao.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amefika katika eneo la Jangwani leo na kushuhudia hali halisi, na kisha kutoa agizo kwa wakuu wa shule kuwa wanafunzi wapumzike nyumbani kwa siku mbili, mpaka hali itakapokuwa nzuri.

Aidha, Makonda amewaomba wakazi waishio maeneo hayo kuchukua tahadhari na kuondoka maeneo hayo kwa kipindi hiki cha mvua ili kuepusha madhara makubwa zaidi kuwatokea.

DCIM100MEDIADJI_0044.JPG
DCIM100MEDIADJI_0040.JPG
DCIM100MEDIADJI_0037.JPG
DCIM100MEDIADJI_0034.JPG
DCIM100MEDIADJI_0030.JPG
DCIM100MEDIADJI_0025.JPG
DCIM100MEDIADJI_0023.JPG
DCIM100MEDIADJI_0020.JPG
DCIM100MEDIADJI_0018.JPG
DCIM100MEDIADJI_0015.JPG
DCIM100MEDIADJI_0013.JPG