ANGALIA MAPACHA WASIOPENDA KULA WAFARIKI DUNIA,WAACHA HUZUNI

Bofya Hapa

Mapacha wawili wanaofanana mno, ambao wamekuwa maarufu kupitia mapambano yao makali dhidi ya ugonjwa wa kukosa hamu ya kula, wamekufa kwa ajali ya moto ulioteketeza nyumba yao. Clare na Rachel Wallmeyer wenye miaka 42, walikuwa baada ya moto kulipuka nyumbani kwao huko Geelong, karibu na Melbourne, mmoja akiteketea kwa moto, mwingine akipata majeraha makubwa ya moto na kufariki muda mfupi baadaye akiwa njiani kupelekwa hospitali.

Lilikuwa ni janga lililokatisha maisha ya ghasia, kwa madada walioonekana kwenye Televisheni ya Australia mara kadhaa kuzungumzia kuhusu ugonjwa wao wa kukosa hamu ya kula ambao uliwafanya wote wawili kukonda na kuishi kama wakiwa kama mifupa mitupu na kuwa tatizo pia kwa wazazi wao, wafanyakazi wa jamii na polisi.

Katika mapitio ya kutia uchungu ya maisha yao walisema katika miaka ya hivi karibuni kwamba hawakuwahi kuwa katika mapenzi, hawakuwahi kupata kazi na wanaamini kwamba ilikuwa wakisubiri tu muda kabla hawajafa, na kwamba watakufa pamoja. Vifo vyao kwenye moto inaaminika kuwa ni ajali ya kawaida, kwa mujibu wa wapelelezi kutoka Kitengo cha Uchunguzi wa Jinai cha Geelong ambao walisema kwamba uchunguzi wa awali haukubainisha matukio yoyote yenye kutia mashaka.

Hatahivyo kumekuwepo na taarifa kwa miaka kadhaa kuhusu wanawake hao kila moja ikidai kwamba wamekuwa wakijaribu kuuana. Rachel alishitakiwa kwa kujaribu kumuua Clare baada ya polisi, ambao waliitwa nyumbani kwao kudai walishuhudia Rachel kwa mikono yake akiwa kamkaba dada yake kooni. Mashitaka hayo baadaye yalifutwa.

Mandatory Credit: Photo by Mike Dugdale/Newspix / Rex Features (1829736a)
Clare and Rachel Wallmeyer with friend and LEAP Chairperson Rachael Walker
Anorexic twins Clare Wallmeyer and Rachel Wallmeyer, Australia – 03 Sep 2006
A pair of anorexic Australian twins have died in a house fire. Rachel and Clare Wallmeyer, 42, became famous after detailing their battle with anorexia on TV. They were killed after a fire broke out at their home in Geelong, near Melbourne, with one dying at the scene and the other in hospital. According to firefighters the blaze is being treated as non-suspicious, though the cause is still being investigated. Neighbours raised the alarm after smelling smoke. Rachel and Clare, who had attempted suicide several times, had previously spoken out about their belief that they would die together. However, their volatile relationship had also seen Rachel accused of trying to murder her sister in 2010.

Uwepo wao, uliwiana kati ya maisha na kifo, ndio ukapelekea kampuni za Televisheni kuwatafuta kwa ajili ya mahojiano baada ya mamlaka husika kufikiria kuwafungia katika harakati za kuwakinga wanawake hao wasijiue kwa njaa na ‘kubadili kabisa maisha yao.’ Claire baadaye alifungwa na Mahakama ya Geelong kwa marukio kadhaa ya wizi, lakini pale Hakimu Ian von Einem kusema hakuwa na jinsi ila kumpeleka jela ili kumuepusha na vitendo vya kutaka kujiangamiza mwenyewe.

Dada yake pia alizipasua vichwa mamlaka pale alipokamatwa kwa kosa la kuendesha gari huku akiwa kalewa dawa za kulevya na alituhumiwa kumsukumia mtu mmoja kwenye njia ya treni. Alihukumiwa kifungo cha miezi 21 jela. Lakini pale walipoanza kupungua uzito katika kipindi cha miaka 20, uzito wa kila mmoja uliporomoka kwa kilo zisizopungua nne.

Madaktari walisema walikuwa na mifupa kama ya wanawake wenye umri wa kati ya miaka 70 na 100. Wazazi wao, Bob na Moya walikiri kwamba mapacha hao walipokuwa chini ya miaka 20 walihofia wangeweza kuwakuta wamefia kitandani kutokana na matatizo yao hayo.

Katika mahojiano kwenye kipindi cha Dakika 60 mapacha walitoa uzoefu wao wa kushitusha kuhusu tabia zao za kula.