ANGALIA MAZISHI YA WINNIE MANDELA,AZIKWA SOWETO JANA,AFRIKA KUSINI SIMANZI

Bofya Hapa

MAZISHI ya aliyekuwa mpiganaji dhidi ya ubaguzi nchini Afrika Kusini, Winnie Mandela yamefanyika leo nyumbani kwake Soweto ambako aliagwa na zaidi ya watu 40,000 waliofuraika katika uwanja wa mpira kushuhudia tukio hilo.

Mazishi hayo yalikuwa ni ya kiwango cha juu zaidi kufanywa kwa mtu ambaye si mkuu wa nchi. Marehemu Winnie ambaye alikuwa mke wa aliyekua rais wa kwanza wa Afrika Kusini baada ya kuanguka kwa utawala wa kibaguzi, Nelson Mandela, alifariki Aprili 2 mwaka huu akiwa na umri wa miaka 81. Rais Cyrille Ramaphosa wa Afrika Kusini aliongoza mazishi hayo pamoja na familia ya marehemu Winnie.

Salaam za rambirambi zimemiminika kutoka kwa viongozi mbalimbali duniani, akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ambaye alimtaja kama “alama ya kimataifa ya kupinga uonevu”. Winnie Mandela alikulia katika jimbo la Eastern Cape kabla ya kwenda kufanya kazi jijini Johannesburg ambako alikuwa na Nelson Mandela na kuoana mwaka 1958.

Wanafamilia.

Rais Ramaphosa akiwa msibani.

Mjane wa Mzee Mandela.

Winnie enzi za uhai wake.

Mtoto wa marehemu.