ANGALIA MTOTO ALIYEKAA HOSPITALI KWA MIEZI 5 BILA MAMA YAKE KISA DENI

Bofya Hapa

February 14, 2018 nimeipata hii kumhusu Mama mmoja ambaye ameelezea furaha yake baada ya zahanati moja ya binfasi kumuachilia mtoto wake mchanga baada ya kuzuiliwa kwa miezi mitano kutokana na kushindwa kulipa bili ya hospitali nchini Gabon.

Mama yake mtoto Angel amesema kuwa maziwa yake yamekauka baada ya kutenganishwa na mtoto wake kwa muda wa miezi mitano. Tukio hilo limewashangaza watu mbalimbali nchini humo ila baadaye mama huyo akapata msaada kutoka kwa Wananchi.

Bili ya dola 3,630 ambazo ni Tsh. Milioni 7 laki 2 na elfu sitini ililipwa baada ya kampeni kuanzishwa kwa niaba ya familia. Rais wa nchini hiyo Ali Bongo alikuwa miongoni mwa wale waliotoa mchango. Mkurugenzi wa kliniki hiyo alikamatwa Jumatatu kwa mashtaka ya kumteka nyara mtoto, lakini mashtaka hayo yakaondolewa baadaye.

Angel baadaye aliachiliwa na kuondoka zahanati hiyo iliyo kaskazini mwa mji muu wiki hii. Baada ya kuachiwa Mama yake mtoto huyo Sonia Okome amesema kuwa amehuzunika kwa kuwa hawezi kumyonyesha mtoto wake kwa sababu maziwa yalikauka. Pia alilalamika kuwa mtoto huyo hajapewa chanjo yoyote.