ANGALIA MTOTO AMBAYE MGUU WANASA KWENYE NGAZI ZA UMEME AIRPORT

Bofya Hapa

Mtoto Julian ambaye mguu wake ulinaswa kwenye ngazi za umeme kwenye uwanja wa ndege wa Vancouver, Canada. Mama yake, Andrea Diaczok, ametoa wito kwa wazazi kuwa macho na watoto wao katika sehemu hizo. MTOTO Julian mwenye umri wa miaka miwili alijikuta akivunjwa mifupa ya mguu wake uliponasa kwenye ngazi za umeme katika kiwanja cha ndege cha Vancouver, Canada.

Kiatu cha Julian kikiwa katika mashine za ngazi za umeme kilipokuwa kimenasa. Julian alikuwa na wazazi wake, Andrea Diaczok, mama yake, na baba yake, Jeff Lee walikuwa wakirejea mjini Calgary wiki iliyopita kutokea Vancouver. Mguu wa mtoto huyo ulikwama pembeni kati ya ngazi na vyuma vinavyozungusha mikanda inayopandisha abiria.

Julian akiwa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu, kinyume na woga wa wazazi wake ambao walifikiri huenda mguu wake ungekatwa. “Mguu wake ulipotea kabisa kwenye mkanda unaozunguka,” Diaczok, alisema na kuongeza kwamba kuona hivyo alipiga kelele kwa nguvu. Wazazi wa Julian wakifurahi naye baada ya matibabu ya mguu wake ambayo yalichukua wiki kadhaa.

Mtambo huo uliukunja mguu wake na kuvunja mifupa ya mguu ambapo kiatu chake kilipotelea ndani ya mkanda huo wenye kuzunguka,” alisema. Kiatu cha Julian kilikuwa kimebanwa kwenye mkanda huo na ilibidi wafanyakazi wa uwanjani hapo na wapita njia kumng’oa mahali hapo aliponasa. Diaczok na Lee ambao ni wafanyakazi katika fani ya afya, walikuwa wamejitayarisha kwamba mwanao angekatwa mguu.

Hata hivyo, madhara hayakuwa makubwa sana, kwani mbali na mifupa iliyokuwa imevunjika na miteguko kadhaa, madaktari waliweza kuhakikisha mtoto huyo anapata matibabu ambayo hayakuwalazimisha kuukata mguu huo. WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA YA HABARI