ANGALIA MWANAMKE ALIYETUPWA JELA KWA KUTUMIA UGONJWA KUFANYA UTAPELI

Bofya Hapa

Binti mmoja nchini Australia ambaye alidanganya kuwa anaumwa ugonjwa wa saratani ili achangiwe pesa na ndugu zake, amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela. Binti huyo Hanna Dickenson, 24, anadaiwa kuchukua Dola za Marekani 31,000 sawa na Shilingi za Kitanzania takribani Milioni 74.4 kutoka kwa wazazi wake na kuwaambia kuwa anakwenda kutibiwa nje ya nchi.

Mahakama imeelezwa kuwa binti huyo alichukua pesa hizo ambazo wazazi wake walizichangisha kutoka kwa ndugu na marafiki zao wa karibu.

Hanna anasemekana kutumia pesa hizo kweye mapumziko wakati wa likizo na kufanyia starehe nyingine.