ANGALIA PICHA MECHI YA KWANZA WANAWAKE KUHUDHURIA TANGU WARUHUSIWE

Bofya Hapa

January 12, 2018 ni siku ya kihistoria katika soka la nchi ya Saudi Arabia baada ya wanawake nchini humo kuhudhuria mechi ya soka kwa mara ya kwanza. Majira ya saa 2:00 usiku kwenye uwanja wa Mfalme Abdullah jijini Jedda wanawake walikuwa tayari uwanjani wakitazama mechi ya ligi kuu kati ya Al-Ahli dhidi ya Al-Batin ambapo Al Ahli ilishinda mabao 5-0. Prince Mohammad Bin Salman Al Saud alitangaza kuwaruhusu wanawake kuingia uwanjani mwezi October 2017. Hata hivyo wanawake wametengewa jukwaa lao “Family sections” ambapo wataruhusiwa kukaa na familia zao bila kuchanganyikana na wanaume ambao si wa familia zao.