ANGALIA PICHA ZA KWANZA KUTOKA ENEO ILIPOTOKEA AJALI MBAYA YA NDEGE NA KUUWA WATU 49

Bofya Hapa

Miongoni mwa stori kubwa Leo March 12, 2018 ni Watu 49 wameuawa na wengine kujeruhiwa baada ya ndege ya abiria ya Bangladesh iliyokuwa na abiria 71 kuanguka wakati ikitua katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Kathmandu nchini Nepal.

Maafisa nchini Nepal wamesema abiria 17 waliokolewa baada ya ajali hiyo huku wengine wengine wakipoteza maisha. “Watu 31 waliuawa papo hapo na wengine tisa wakapoteza maisha wakiwa hospitalini jijini Kathmandu,” -Msemaji wa Polisi Manoj Neupane.

Ndege hiyo ilikuwa imetokea jijini Dhaka, ikielekea jijini Kathmandu. Moto mkubwa na moshi mzito ulishuhudiwa pindi tu ndege hiyo ilipoanguka na maafisa wamekuwa na kazi ngumu ya kujairbu kuuzima ili kuona iwapo itawaokoa abiria.