ANGALIA SABABU ZA A BOY FROM TANDALE YA DIAMOND KUZINDULIWA KENYA

Bofya Hapa

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameongea Exclusive na Bongo5 sababu iliyomsukuma kwenda nchini Kenya kuzindua album yake ya ‘A BOY FROM TANDALE’ badala ya kuzindulia hapa Tanzania kama wasanii wengine wanavyofanya.

Diamond Platnumz amesema sababu kubwa iliyofanya azindulie Kenya album yake ya ‘A BOY FROM TANDALE’ ni kuimarisha mshikamano wetu kati ya Tanzania na Kenya kama ndugu tena kwa vitendo na sio kwa maneno kama baadhi ya watu wanavyoongea.

Hata hivyo, Ijumaa hii Machi 14, 2018 kutakuwa na Listen Party ya album ya ‘A BOY FROM TANDALE’ ambapo kwa mara ya kwanza mashabiki na wadau wa muziki Tanzania watapata nafasi ya kusikiliza album hiyo inayosubiriwa kwa hamu.