ANGALIA WANANDOA WALIOISHI MIAKA 93 YA NDOA

Bofya Hapa

Hali hii inaweza kushangaza kidogo, lakini ndiyo hivyo hutokea hasa pale wawili wanapokubaliana, kuaminiana na kupendana na Mungu akiwa upande wao. Katika hali ya kushangaza na kustaajabisha wanandoa nchini Uingereza wameadhimisha miaka 90 ya ndoa yao jambo ambalo limekuwa kivutio kwa watu wengi nchini humo.

Wanandoa hao Mwenyezi Mungu amewajalia kupata watoto 8, wajukuu 27 pamoja na vitukuu 23, huku wakibahatika mara kadhaa kukutana na Malkia wa Uingereza. Karam na Kartari Chand, wenye umri wa miaka 110 na mwingine 103, wanaaminika kuwa wanandoa waliokaa pamoja kwa muda mrefu zaidi nchini Uingereza.

Inadaiwa kuwa ndoa hao walifunga ndoa nchini India mwaka 1925, wakati binti akiwa na miaka 13 na kuhamia nchini Uingereza miaka 40 baadaye.