ANGALIA WATU 20 WALIOUAWA KWENYE JARIBIO LA WAFUNGWA WAKIJARIBU KUTOROKA GEREZANI

Bofya Hapa

Kutoka Brazil, takribani wafungwa 19 na askari mmoja wa gereza la Santa Izabel Prison Complex wameuawa katika jaribio la wafungwa hao kutoroka gerezani. Inaripotiwa kuwa wafungwa hao waliotaka kutoroka walikuwa wanasaidiwa na kikundi kilichokuwa na silaha nje ya gereza hilo kilichotumia vilipuzi kubomoa ukuta mmoja wapo wa gereza.

Vurugu hizo ambazo zimetokea katika Mji wa Belem zimesababisha vifo hivyo huku askari wengine wanne wakijeruhiwa na moja akijeruhiwa vibaya sana.