Anthony Joshua ampa Rashford mbinu za kuimaliza Liverpool

Bofya Hapa

              Kinda wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester United, Marcus Rashford ametembelea kambi ya bondia wa uzito wa juu Anthony Joshua. Rashford amekwenda kambini kwa bondia huyo wakati timu yake ya Manchester United inajiandaa na mchezo wake wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Liverpool wikiendi hii.

 

Manchester United itasafiri kwenda Anfield siku ya Jumamosi kucheza na Liverpool wakati mashetani wekundu wa Old Trafford wakitaka kuhakikisha wanalinda rekodi yake ya kutopoteza mchezo wake wa nane wakati Jurgen Klopp atahitaji kuhakikisha wanasalia katika nne bora katika msimamo wa ligi. Straika huyo wa United alikwenda na kaka yake katika kambi ya mazoezi ya Joshua ambaye anajiandaa na mchezo wake dhidi ya Kubrat Pulev Oktoba 28.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.