ANTONY JOSHUA BONDIA TYSON ATANGAZA KURUDI ULINGONI MWAKANI

Bofya Hapa

                                 Bondia Tyson Fury ameelezea nia yake ya kurejea ulingoni mwakani ikiwa ni wiki moja tu baada ya kusema hataomba leseni mpya Bodi ya Umiliki wa Masumbwi Uingereza. Fury hajapigana tangu amalize utawala wa Wladimir Klitschko wa muda mrefu kuwa bingwa wa uzito wa juu duniani mjini Dusseldorf mwezi Novemba mwaka 2015. Kufuatia kuwa nje kwa sababu za maumivu kwanza na baadaye kufungiwa kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu, bondia huyo mwenye umri wa miaka 29 kwa sasa hana leseni baada ya kupokonywa kwa kesi ya utumiaji dawa zilizopigwa marufuku michezoni. Lakini wiki moja tu tangu aseme hataomba kurudishiwa leseni na BBBoC, Fury ametweet:

Kuwa tayari kupambana April mwaka 2018 katika pambano kubwa! & tena kwenye majira joto katika pambano kubwa! & tena kurudi mwishoni mwa mwaka. Mapambano matatu makubwa 2018. Fury, 29, has not fought since dethroning Wladimir Klitschko in Dusseldorf in November 2015 Hii si mara ya kwanza Fury anatangaza kurejea ulingoni. Mfalme huyo wa zamani wa uzito wa juu duniani, ambaye alilazimika kuachia mikanda yake kufuatia matatizo yake nje ya ulingo, alirudi gym mapema mwaka huu kwa lengo kubwa la kupigana na Muingereza mwenzake, Anthony Joshua.

Lakini mipango hiyo ilizimwa na tuhuma zake za kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni na hadi sasa hana leseni. Fury was back between the ropes last month for cousin Hughie’s fight against Joseph Parker Dondosha comments