BARAZA LA MAWAZIRI LA MNAGANGWA AJAZA WANAJESHI WALIOMUONDOA MUGABE

Bofya Hapa

RAIS mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa ametangaza Baraza jipya la Mawaziri, ambalo ndani yake amewaweka maofisa wa Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo waliomuunga mkono tangu awali huku pia akiwabakisha mawaziri wengi wa kipindi cha Robert Mugabe.
Mnangagwa amamteua Jenerali Sibuso Moyo, kuwa waziri wa mambo ya nje, Moyo ndiye aliyejitokeza kwenye Televisheni ya Taifa baada ya jeshi kuingilia kati kufuatia hali ya nchi hiyo na kufanya mazungumzo na Mugabe kabla ya kuachia madaraka.Aidha, amemteua kiongozi wa Jeshi la Anga, Perence Shiri kuwa Waziri wa Kilimo na Ardhi huku akiwabakisha maawaziri wengi waliokuwemo kipindi cha Mugabe.Amewapa Wizara viongozi wa chama cha waliopigana vita ya ukombozi waliokuwa wakimuunga mkono wakiongozwa na Chris Mutsvangwa amepewa Wizara ya Habari.Mkosoaji wa Serikali Tendai Biti amesema kuwa Wazimbabwe walikosea kudhani kungekuwa na mabadiliko yoyote huku akisema kuwa fungate iliokuwa ikisherehekewa Zimbabwe imeisha kabla ya kuanza.Upinzani umelaumu mabadiliko hayo kama usaliti wa matumaini miongoni mwa raia na thibitisho kuwa vikosi vya usalama vilivyokuwa na nguvu nyingi wakati wa utawala wa Mugabe vinaendelea kuthibiti taifa hilo.Hali ya kuleta uwiano na umoja ilioonekana katika siku za karibuni huenda ikabadilishwa na makabiliano ya uongozi katika uchaguzi wa mwaka ujao.