BREAKING: ABDUL NONDO KUPELEKWA MAHAKAMANI, SIMU YAKE YAFICHUA MAMBO MAZITO

Bofya Hapa

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa kauli kuhusu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo (24) aliyedaiwa kutekwa wiki iliyopita, kuwa si kweli kwamba alitekwa, bali alisambaza taarifa za uongo na kwamba alikuwa anakwenda Iringa kumtembelea msichana mmoja ambaye jina lake halijawekwa wazi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar. “Huyu mwanafunzi aliyedai kutekwa si kweli, kuna mawasiliano ambayo tumeyakamata alikuwa akifanya na binti mmoja ambaye ndiye alikuwa anamfuata huko Iringa.

Alipatikana akiwa mzima wa afya akiendelea na shughuli zake za kawaida, alipelekwa kwa daktari kupimwa na kukutwa hana tatizo lolote la akili.