CHECK WATU WALIOKAMATWA WAKIUZA MISHIKAKI YA NYAMA ZA BINADAMU,NI UKATILI WA KUTISHA

Bofya Hapa

Wabrazili wanaokula nyama za binadamu wamewapika watu waliokuwa wakiwashikilia na kuwachoma mishikaki kwa ajili ya kuuza katika tukio la kutisha na kusisimua, Polisi wamegundua jana. Mtaalamu wa Kareti Jorge Beltrao Negromonte mwenye miaka 55, mkewe Isabel Pires mwenye miaka 51 na mfanyakazi wao Bruna da Silva, waliwarubuni wanawake kwenye nyumba yao kwa ahadi ya kuwapatia kazi za ndani.

Kisha watuhumiwa hao watatu wakawaua wanawake hao na kutumia nyama zao kutengeneza mishikaki maarufu inayojulikana kama ’empanadas’ ambayo waliwauzia majirani zao mjini Pernambuco, katika eneo lililoko Kaskazini mwa nchi hiyo, wamesema polisi. Vidhibiti vya tukio hilo la kutisha vimegundulika wiki iliyopita baada ya maofisa wa polisi kupitia kitabu chenye kurasa 50 kinachomilikiwa na Da Silveira, kilichohusisha michoro na taarifa za ulaji nyama za binadamu.

Polisi wamegundua miili miwili katika bustani iliyoko kwenye nyumba inayomilikiwa na kundi hilo. Wanaamini kuwa miili hiyo iliyopatikana ni ya Alexandra Falcao mwenye miaka 20 na Gisele da Silva mwenye miaka 30 ambao waliripotiwa kupotea eneo hilo hivi karibuni. Wanawake wawili walionekana wakirandaranda kwenye nyumba ya watuhumiwa kabla ya kutoweka. Mauaji hayo yanafanana na yale yaliyofanywa na kinyozi Sweeney Todd ambaye aliwafunga kamba mateka wake kwenye duka lake eneo la Fleet Street. Mshirika wa Todd kwenye kesi hiyo, Bi Lovett alimsaidia kuteketeza miili hiyo kwa kuzioka nyama zao katika vipande vidogo na kuuza kwa wateja wasiotiliwa mashaka dukani mwake.

Walanyama za binadamu wanaamini katika kundi la watu wanaoabudu ‘usafishaji wa dunia na upunguzaji wa idadi ya watu’, Inspekta Wesley Fernandes wa mji wa Garanhuns alisema. Fernandes alisema, watatu wamekamatwa Jumatano iliyopita na wamekiri mashitaka yao. aliongeza kuwa walipanga kuua wanawake watatu kila mwaka. Wamedaiwa kuwa tayari walishapanga mauaji ya mwanamke mmoja anayeishi jirani na Jiji la Lagoa do Ouro.

Watuhumiwa hao walisema wamewateka wanawake hao kwa kishawishi cha kuwatafutia kazi za majumbani. Waliweza kugundulika baada ya mmoja wa wanawake hao kutumia kadi ya manunuzi inayomilikiwa na mmoja ya watu walioripotiwa kupotea mwezi uliopita. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Brazili, majirani wa watuhumiwa hao watatu walichoma moto nyumba ambayo ilipatikana miili Alhamisi.

Kamishna wa Polisi Wesley Fernandes alisema watuhumiwa hao watatu walipanga kuua mwanamke mwingine wa mji jirani, na kufikiria kuua wengine zaidi mjini humo.