CHIRWA AIONDOA YANGA MAPINDUZI CUP, URA YATINGA FAINALI

Bofya Hapa

Ikiwa ndiyo siku ya kwanza anaichezea Yanga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, mshambuliaji Obrey Chirwa amekosa penalti ya mwisho na kuing’oa Yanga katika michuano ya Mapinduzi. URA ya Uganda imeitoa Yanga kwa mikwaju 5-4 na kufanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mapunduzi.

Mwaka 2016, URA iliing’oa tena Yanga katika hatua hiyo kwa mikwaju ya penalti. Chirwa alikuwa amegoma kujiunga na Yanga akitaka alipwe fedha zake za usajili. Lakini leo ameungana na kikosi hicho akitokea Dar es Salaam.

Ikiwa ndiyo siku ya kwanza amejiunga na Yanga, Chirwa alitokea benchi kuchukua nafasi ya Pius Buswita na dakika 90 zikaisha kwa sare ya bila mabao, ikaingia mikwaju ya penalti. Chirwa ndiye alikuwa wa mwisho upande wa Yanga baada ya Papy Tshishimbi, Hassan Kessy, Raphael Daud na Gadiel Michael kupata.