DIAMOND PLATINUMZ AMTOA MACHOZI NISHA,NI BAADA YA KUINGIZWA MJINI TENA

Bofya Hapa

Wimbo wa msanii Diamond Platnumz ‘Sikomi’ umeukonga moyo wa muigizaji Nisha kiasi kwa mrembo huyo kububujikwa na mazozi.

Wimbo huo ambao maudhui yake unazungumzia mapenzi kwa mtu ambaye ametendwa, unasikika katika video ambayo ameiposti Nisha katika ukurasa wake wa Instagram ambapo anaonekana akilia.

Hivi karibuni kumekuwa na stori kuwa aliyekuwa mpenzi wa Nisha kwa sasa anatoka kimapenzi na msanii Snura, hata hivyo muimbaji huyo amekuwa akikanusha hilo kwa kueleza wapo pamoja kikazi tu na si vinginevyo