DIAMOND PLATINUMZ MAPYA TENA,PENNY AFUNGUKA KUHUSU CHIBU,WAKATI MAUA YAKITIKSA MITANDAO

Bofya Hapa

Penny- Ningemzalia Diamond Lakini Alikuwa Hajatulia Mtangazaji maarufu Penny au maarufu kama Vj Penny amefunguka kuhusu uhusiano wake na staa wa Bongo fleva, Diamond Platnumz ambapo amekiri kuwa endapo angekuwa ametulia angemzalia.

Penny na Diamond walikuwa na uhusiano wa kimapenzi miaka michache iliyopita na kuna wakati ilisemekana kuwa Penny alikuwa amembebea mimba Diamond lakini baadae habari zilienea kuwa alichoropoa mimba hiyo. Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda Penny amefunguka kuwa sababu iliyomfanya mpaka hakuzaa na Diamond kipindi cha Mahusiano yao ni kutotulia kwake:

Mimi napenda sana mtoto ndoto yangu ni siku moja nije kuwa mama lakini pia nataka mwanaume ambaye nitazaa naye awe baba bora kwa mwanangu. Kwa kipindi kile niliposhika mimba ya Diamond siwezi kusema sana kuhusu yeye lakini ningeweza kumzalia lakini alikuwa ana mambo mengi”. Lakini pia Penny alipoulizwa anamshauri Diamond amuoe nani kati ya Wema na Zari kwani alitangaza kuoa mwaka huu Penny alifunguka:

Kwanza yeye aangalie mwanamke anayempenda kwa dhati, anayejua familia na kumshauri vyema katika kazi zake na pia asithamini sana starehe badala ya maendeleo”. Penny amesisitiza kuwa kamwe hawezi tena kurudiana na Diamond kwani kila mtu ameshakuwa na maisha yake na yeye ana mpenzi wake.