Haji Manara na Shaffih Dauda watangaziana vita,

Bofya Hapa

Baada ya Klabu ya Simba jana jumatatu Januari 9, 2018 kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi naKlabu ya URA. Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara na Mchambuzi wa michezo wa kituo cha Radio Clouds FM, Shaffih Dauda wameingia kwenye vita kali ya kurushiana maneno. Haji Manara na Shaffih Dauda Choko choko ilianzia pale Simba SC ilipofungwa, ambapo Shaffih alianza kuposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akihoji kuhusu mwenendo wa klabu hiyo tangu ulipoanza mwaka 2018.

 

Shaffih alianza kuposti picha mbalimbali za Simba SC na kuuliza kama kuna uwezekano wa klabu hiyo kukwea ndege msimu ujao akiimanisha kufuzu kushiriki michuano ya kimataifa huku akihimiza mabadiliko ndani ya timu hiyo kuwa yaanzie kwa Haji Manara kwani ndiye anayewapotosha mashabiki wa Simba SC. Uvumilivu ukamshinda Haji Manara ndipo alipoamua kumtolea uvivu Shaffih Dauda kwa kumwambia kuwa chuki zake binafsi na klabu ya Simba asiwaambukize mashabiki wengine kwa kuposti vitu vya kichochezi na kumuonya kuwa endapo ataendelea basi atamuadabisha yeye pamoja na Radio Clouds FM.

Tunajua wewe una ugomvi wako binafsi na baadhi ya viongozi wa Simba. Lakini usitafute ugomvi na wanasimba wote, Sie kufungwa sio wa kwanza na hatutakuwa wa mwisho. Unatumia muda mrefu kuittack Simba na post zako za kijinga. Tunajua unajikomba kwa Yanga baada ya kutaka kukupiga kwenye issue ya Akilimali, jipime bro vinginevyo utavunja heshma yako na ya clouds media pia.”ameandika Haji Manara. Shaffih Dauda naye akaona sio vyema kukaa kimya akaamua kumjibu kwa kumwambia Manara asimtumie yeye kama kichaka cha kujificha, Kwani Simba ilipofungwa na Green Worriors Manara alitumia kichaka cha Omog kuficha makucha.

 

Kaka usinitumie mimi kichaka cha wewe kujifichia, last time Simba imefungwa na Green Worriors uljifichia kwa Omoga katimuliwa sasa hivi hauna mahala pa kujifichia.“ameandika Shaffih Dauda na kumtaka Haji Manara ajiuzulu nafasi yake “Ilibidi wakati huu unaozungumza uwe umeachia nafasi yako kwasababu umekuwa ukiwadanganya kwa kuwapa matumaini hewa wana Simba.“amemaliza Shaffih Dauda.

Hata hivyo mashabiki wengi wa Simba SC wamemshambulia Shaffih Dauda kwa kumuita mchochezi na wengine wakimtaka kutomshambulia Manara amuache afanye kazi yake huku baadhi ya watu wakimshauri Shaffih aendelee kufanya kazi yake ya uchambuzi aachane na uongozi wa Simba.