HAMISA MOBETTO AMTIBUA TENA ZARI THE BOSS LADY ,AYAAMSHA YALIOLALA

Bofya Hapa

        KILA kukicha mambo yanazidi kupamba moto kwa wanawake wawili waliozaa na staa wa muziki Bongo huku Hamisa Mobeto akionekana kuyaamsha yaliyolala kwa mwenzake, Zarinah Hassan, mjasiriamali kutoka Uganda aliyezaa watoto wawili na msanii huyo. Hamisa alionekana kuyaamsha yaliyolala kwa Zari baada ya Wikiendi iliyopita kuweka kwenye ukurasa wake wa Instagram video ya zamani iliyoonyesha tangazo la godoro na vitu mbalimbali waliyofanya wawili hao, yakikumbushia maneno yaliyozagaa wakati huo kuwa aliacha hereni chumbani.

 

               Chini ya video hiyo, Hamisa aliandika maneno haya; “It’s about time nifuate hereni zangu…. I hope they are still there,” ambapo aliamsha hisia za mashabiki wake huku wengine wakimshambulia kwamba huenda amepewa fedha au wanafanya kiki huku wengine wakienda mbali zaidi na kusema inawezekana hata kumpeleka mahakamani msanii huyo ni kiki. “Hapa kuna mchezo wanatuchezea hawa, inawezekana kabisa wako pamoja na huyo msanii wanalea mtoto wao vizuri na ile ilikuwa ni janja tu ya kumdanganya Zari huku wakiendelea na mapenzi yao kama kawaida,” aliandika mmoja wa wadau kwenye mtandao huo.

 

                  Huyu Hamisa anatakiwa ajifunze kunyamaza maana anashindana na Zari ambaye hana hata muda naye, akae awaze atafanya nini ili alee mtoto wake, lakini badala ya kuwaza hayo yeye kutwa kucha ni mambo ya mwanaume huyo tu, kama umaarufu tayari anao yeye kama mwanamke anatakiwa apigane kufanya hata biashara kwenye mtandao maana ana wafuasi wengi watanunua tu na ataweza kumlea mwanaye vyema,” aliandika mdau mwingine.

 

        Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mobetto ili kuelezea kwa nini amekuwa akimchokonoa Zari mara kwa mara lakini jitihada hizo ziligonga mwamba na hata alipopigiwa mama yake alisema hawezi kuzungumza chochote na waandishi.