IGP SIRRO AMUAPISHA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR

Bofya Hapa


Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akimuapisha kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassani Haji, leo Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam, baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassani Haji, akiweka saini hati ya kiapo baada ya kuapishwa na Mkuu wa Jeshi hilo IGP Simon Sirro, Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es salaam, Kamishna Haji aliteuliwa na Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassani Haji, akitoa neno mbele ya Maofisa Wakuu Waandamizi na askari wa vyeo mbalimbali (hawapo pichani) baada ya kuapishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, kuwa kamishna wa Polisi Zanzibar huku akiahidi kufanyakazi kwa uzalendo na kumsaidia IGP Sirro katika majukumu ya kulinda usalama wa raia na mali zao.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, na Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassani Haji, wakiwa katika picha na Maofisa wa Jeshi hilo baada ya hafla ya kumuapisha kamishna wa Polisi Zanzibar kukamilika leo Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es salaam.

Picha na Jeshi la Polisi.