JACKLINE WOLPER KUTIKISA DAR NA DODOMA,KUFANYA PARTY YA AJABU

Bofya Hapa

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper, leo anatarajia kufanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa huko Masaki katika ukumbi wa Buckets ambapo atazindua ‘Application’ ambayo itapatikana kwenye Google Play Store ya duka lake la nguo kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa ukaribu. Wolper akiwa kwenye pozi. Msanii atakayepiga shoo katika hafla hiyo ni Barnaba Classic kuanzia saa moja mpaka saa sita usiku. Wolper amemchagua Barnaba kupiga shoo hiyo kwa kuwa ni msanii anayempenda na kumsapoti kwa ukaribu akisema nyimbo zote alizoimba zinaelezea maisha yake aliyoyapitia. Staahuyo amewaomba mashabiki zake kufika kwa wingi katika ukumbi wa Buckets kumsapoti na amesema kiingilio ni shilingi 10,000/- tu. Wasanii mbalimbali wengine watakuwepo kumsapoti Wolper leo. Pia amesema shangwe za siku yake ya kuzaliwa zitaendelea kesho mjini Dodoma katika klabu ya usiku ya burudani ya Maisha. Amewaomba pia mashabiki zake wa mji huo kujitokeza kwa wingi kumsapoti. Kampuni ya Global Group tunamtakia Wolper kila la heri katika siku yake ya kuzaliwa. (HABARI: NICOLAUS TRAC | GLOBAL PUBLISHERS)