Jaguar azichapa na mbunge mwenzie Bungeni

Bofya Hapa

    Wabunge vijana wawili wa Kenya jana wamepigana bungeni kutokana na tofauti ya vyama vyao na viongozi wanaowaunga mkono. Wabunge hao ni msanii maarufu Charles Njagua maarufu kama Jaguar na Paul Ongili maarufu kama Babu Owino.

 

Ilikuwa hivi kabla ya kikao cha jioni kuanza Babu Owino aliingia kwenye chumba cha waandishi wa habari na kuwasalimia kisha akaenda kwenye ofisi ya ofisa uhusiano wa bunge. Muda mfupi baadaye Jaguar akaingia kwenye chumba cha waandishi na kuuliza “Huyu Babu yuko wapi?” Babu Owino akatokea na wakaanza kurushiana makonde na kutoleana maneno makali kabla ya kutenganishwa na maofisa wa bunge. “Tutakufundisha adabu Babu, lazima umuheshimu Rais,”alisema Jaguar ambaye ni Mbunge wa Starehe.

 

Akijibu kwa hasira Babu Owino ambaye ni Mbunge wa Embakasi Mashariki alimuuliza Jaguar “Rais yupi? Rais pekee ninayemjua ni Raila Odinga.” Hata hivyo maofisa wa bunge walifanikiwa kuwatenganisha na wabunge hao watafikishwa kamati ya bunge ambapo wanaweza kuzuiwa kuhudhuria baadhi ya vikao vya bunge.