JAY Z AKIRI KUMSALITI BEYONCE

Bofya Hapa

Hiphop Super Star Jay Z ambaye pia ni Mume wa Mwimbaji staa Beyonce amezungumza na jarida la The New York Times Style na kusema kuwa anakubaliana na tuhuma zilizokuwa zikidai alimsaliti Beyonce mwaka 2013.
Solange ambaye ni mdogo wake Beyonce alionyesha kutofurahishwa na kitendo hicho na kuhusishwa kumpiga vibao Jay Z wakiwa wote kwenye lifti ndani ya jengo moja New York.

Jay Z amethibitisha hilo kwenye album yake ya 4:44 ambapo aliimba baadhi ya mistari kwa ajili ya kumuomba msamaha Beyonce na kuliambia jarida hilo la The New York Times Style kuwa hakuna kitu kigumu kama kuona sura ya mtu imejawa na maumivu uliyoyasababisha wewe.
Amesema ilifikia mahali walitaka kupeana talaka lakini alipata tiba iliyomsaidia kupita katika wakati huo mgumu na sasa wanaendelea vizuri kwenye maisha ya ndoa ambayo imezaa watoto watatu.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.