KAKA YAKE MESSI MBARONI BAADA YA BUNDUKI KUKUTWA KWENYE BOTI YAKE

Bofya Hapa


Matias Messi.
KAKA mkubwa wa nyota wa soka, raia wa Argentina, Lionel Messi, amekamatwa baada ya kukutwa na bunduki isiyokuwa na kibali na boti yake ya mashindano ikiwa imetapakaa damu.
Imeripotiwa kwamba Matias Messi (35) alitiwa mbaroni jijini Rosario, Kaskazini mwa Argentina akiwa anatibiwa taya lililoteguka na majeraha mengine ambayo anadai yalitokanana ajali aliyopita katika boti hiyo.
Damu zilivyotapakaa kwenye boti.
Matias amesema aliteguka taya na kupata maumivu ya pua baada ya kujipigiza katika ukingo wa ardhi wakati anaendesha boti hiyo katika Mto Panama.
Hata hivyo, katika uchunguzi wao, polisi walikuta bastola kwenye boti hiyo ambayo nayo ilikuwa ina madoa ya damu, hivyo kumkamata.
Vyombo vya habari vya Argentina vimeripoti picha ya boti iliyotelekezwa kwenye eneo la kuvulia samaki huko Fighiera, karibu na nyumbani kwa Matias huku ikielezwa kuwa endapo atapatikana na hatia anaweza kufungwa hadi miaka sita jela.
Hiyo sio mara ya kwanza kwa Matias kuingia kwenye tuhuma mbaya kama hizo ambapo mwaka jana aliwekwa selo kwa saa 16 baada mwaka juzi 2015 kukutwa na bunduki 22 ndani ya gari lake zikiwa hazina kibali, mwaka 2008 alikamatwa na bunduki kwenye mkanda wake wa suruali.

Kwa upande wa familia ya Messi na mwanasheria wake, Ignacio Carbone wanasema ndugu yao hajakamatwa na hizo bastola bali ni tukio la kutengenezwa huku polisi wakisema wamefanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa bunduki hizo zimekutwa kwenye boti yake.
Utafiti ulianza Alhamisi baada ya wanakijiji kumkuta Matias akiwa na majeraha katika penezoni mwa mto Panama, umbali wa maili 20 Kusini mwa Rosario.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Hospitali aliyotibiwa, Carlos Lovesio amethibitisha kuwa Matias amefanyiwa upasuaji wa taya, pua na maeneo mengine ya uso alikojeruhiwa.

Lionel Messi na kaka yake Matias Messi.