KAPOMBE AANZA KUPIGIA HESABU MAKUNDI CAF

Bofya Hapa

BEKI wa Simba, Shomary Kapombe, ameanza kupigia he­sabu za kupambana kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kusema kuwa, wanakwenda Misri kumalizia kazi ya ku­waondoa Al Masry. Kapombe amesema hivyo ikiwa Jumamosi ijayo timu hizo zinatarajiwa kucheza mechi ya marudiano ya michuano hiyo baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa Jumatano iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar kumalizika kwa sare ya 2-2.

Katika mchezo huo, Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa John Bocco, Al Masry wakasa­wazisha kwa bao la Ahmed Gomaa, kisha wakaongeza la pili lililofungwa na Mo­hammed Abdalraof, kabla ya Simba kusawazisha kupi­tia kwa Emmanuel Okwi. Keshokutwa Jumatano, Simba inatarajiwa kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo huo wa marudi­ano utakaopigwa kwenye Uwanja wa Port Said.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kapombe alisema: “Kwa jinsi tulivyocheza hapa nyumbani, naamini kabisa tutaenda kufanya vizuri katika mechi ya marudiano na ku­songa mbele. “Malengo yetu ni kuona tunaingia hatua ya makundi ya michuano hii na kufika mbali zaidi, hivyo hatutakuwa tayari kuona tunaipoteza nafasi hii tuliyonayo.” Omary Mdose, Dar es Salaam.