KAULI YA KWANZA YA MAM WA MTOT ALIYEBAGULIWA NA H&M

Bofya Hapa

Baada ya ubaguzi wa rangi kufanyika kwa mtoto wa kiume na kampuni ya nguo ya H&M kwa kumvalisha nguo yenye maneno ya kudhalilisha watu weusi yanayosema “Coolest Monkey in the Jungle” yakimaanisha “Mimi ni nyani mtulivu msituni

Mastaa kadhaa kutokea Marekani walichukizwa na kitendo hicho kilichofanywa na kampuni hiyo ya H&M akiwemo P.Diddy, T.I huku THE WEEKEND akitaka kujitoa katika mkataba wa kufanya kazi na H&M baada ya kuona kitendo hicho cha kibaguzi. Kupitia mtandao wa instagram maneno ya mama mzazi wa mtoto huyo yamewashangaza wengi baada ya mama mzazi wa mtoto huyo kuwataka watu waache kulia muda wote kutokana na ishu hiyo ya mwanae kwamba haina ulazima wa kuiongelea kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya maneno ya mama huyo watu wengi wametafsiri kuwa huenda akawa hampendi mwanae au hajali kwa unyanyasaji aliofanyiwa mwanae, wengi wamehisi kuwa huenda kampuni ya H&M imempa pesa mama huyo ili kujisafisha na kulifanya suala hilo lionekane la kawaida.