KESI YA MASOGANGE YANGURUMA TENA LEO, MAPYA YAJIRI,YAKWAMA KISUTU

Bofya Hapa

                       Kesi ya kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na wakili wa utetezi wa mtuhumiwa kuchelewa kufika mahakamani hapo.

Kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri imepangwa kusikilizwa tena Novemba 14, mwaka huu.