LADY JAY DEE AIBUKA,AWALIPUA WASANII WA BONGO

Bofya Hapa

              Msanii wa Bongo Flava, Lady JayDee amefunguka kwa kusema kuwa watanzania tunapenda kutukuza vitu vya nje kuliko vya kwetu. Lady JayDee amesema kuwa tofauti na nchi nyingine, Watanzania tumekuwa tukitukuza muziki wa nje na kuacha muziki wetu ukikosa dira na nafasi ya kupigwa kwenye Media za nje.

 

Tofauti ni kwamba watu wengine wanakubali muziki wao kwao na hawatoi nafasi sana na nakipaumbele cha muziki wa nje kama ambavyo sisi tunafanya, Na tatizo letu ni kwamba tunashobokea sana muziki wa nje kuliko muziki wa nyumbani“,amesema Lady Jay Dee kwenye mahojiano yake na kituo cha Radio cha A-FM cha mjini Dodoma kupitia kipindi cha The Finest.

 

Kwa upande mwingine Lady JayDee amesema muziki wetu huwa unakumbwa na upepo wa muziki wa aina fulani kutoka nje kama Afrika Kusini na Nigeria kitu ambacho kinasababisha muziki wetu kukosa ladha. Lady Jay Dee na mpenzi wake Mnaijeria,

 

Spicy wapo mkoani Dodoma ambapo leo Eid Mosi watawasha moto ndani ya kiota kipya cha burudani mjini humo, Capetown Kisasa, na kwenye show hiyo watasindikizwa na mkali wa singeli Msaga Sumu na Nay wa Mitego.