LULU AKIWA GEREZANI MIEZI 3 SASA,MAPYA TENA YAANIKWA,MAMA YAKE ANENE

Bofya Hapa

Ikiwa takribani miezi 3 sasa, tunaambiwa Lulu amenenepa huko gerezani kwa kukubaliana na hali halisi na hajawahi kuumwa. Afisa mmoja wa magereza akichonga na globalpublishers amesema Lulu ndie amegeuka kuwafariji wanaoenda kumtembelea hasa ndugu zake badala ya wao kumfariji.

Lulu amekuwa akiwaambia wasijisikie vibaya hakuna aijuaye Kesho yake na yeye wachukulie Kama yupo shule Ya Boarding kuna siku atakuwa Huru . Munalove aliyeanzia kuigiza Kaole ambaye amekuwa na Lulu kwa mvua na jua kwa Miaka mingi sasa ambapo hakosi kwenda gerezani kumuona lulu Kila wiki, alipoulizwa na GPL alisema . .

“anatushangaza hata sisi, kwanza kanenepa na anaonekana mwenye furaha maana wakati mwingine tukienda kumuona tunakuwa na simanzi lakini yeye anakuwa mfariji wetu akisema kwamba ipo siku atatoka na kuwa huru tena,” . .

Mama Lulu yeye alipopigiwa simu na GPL aliwaka kwa kuja juu akisema hataki kabisa kusikia magazeti wala waandishi wa habari kwakuwa yeye sio superstar, ameomba Lulu aachwe kwakuwa yupo gerezani, alikataa kabisa kutoa maelezo kuhusu binti yake huyo aliyejipatia umaarufu mkubwa akiwa mdogo kuliko umri wake .