MAMA KANUMBA AOHOFIA VITUKO VYA LULU AKITOKA JELA,AFUNGUKA HAYA LULU AKIWA GEREZANI

Bofya Hapa

Mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema Elizabeth Michael ‘Lulu’ anaweza kutoka gerezani na kumezesha maneno machafu juu yake. Mwigizaji huyo alihukumiwa na mahakama jela miaka 2 baada ya kukutwa na hatia za kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake, Steven Kanumba.

Frola ameliambia Gazeti la Mwanaspoti kwamba, binti huyo akirudi anaweza kumezeshwa maneno mabaya akaanza kumshambulia kama awali ambazo anadai kipindi cha nyumba aliwahi kuitwa kubwa jina na binti hiyo. “Mtoto wangu huyu anaweza kurudi mtaani na kushikwa masikio tena na watu kunifanyia vibweka kama alivyofanya awali, wala asithubutu wala kujihangaisha kwa kuwa iliyomshtaki ni Jamhuri hivyo anapaswa kuniheshimu,” anasema.

“Hakuna neno lililoniuma kama siku aliyonipigia na kuniita kubwa jinga huku akiniambia haogopi polisi wala mahakama,” aliongeza Mama Kanumba. Flora anasema kama mzazi anamwonea huruma Lulu na anatamani kumtembelea gerezani na kumpa moyo, lakini kama ndugu zake watakuwa tayari japo hawezi kulazimisha hilo kukubaliwa.