Mchezaji Juma Nyosa Aingia Matatani Tena Baada ya Kumshushia Kipigo Shabiki Mpaka Kuzirai Leo

Bofya Hapa

KAITABA: Jeshi la Polisi linamshikilia Beki wa Kati wa Klabu ya Kagera Sugar, Juma Nyoso kwa tuhuma za kumpiga shabiki hadi kuzirai

Inadaiwa kuwa Mchezaji huyo alikerwa na maneno(matusi) ya Mashabiki ndipo alichukua uamuzi huo wa kumshambulia mmoja wao Majeruhi huyo ameondolewa Uwanjani hapo(Kaitaba) kwa gari maalum la kubebea Wagonjwa(Ambulance)

Ikumbukwe kuwa Mchezaji huyo wakati akiichezea Mbeya City aliwahi kuadhibiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini(TFF) kwa kosa la kumdhalilisha kwa kutumia kidole cha kati Mshambuliaji, John Bocco(aliyekuwa akiichezea Azam FC)