Mkali wa Country Music, Loretta Lynn apata nafuu

Bofya Hapa

Muimbaji na muandishi wa mashairi kutokea marekani anayefahamika zaidi na ngoma zake kama Coal Miner’s Daughter iliyotoka mwaka 1970 na kufanya vizuri ameruhusiwa hospitali’ Mwanamama huyo alilazwa hospitali kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi. Taarifa za kulazwa kwake zilitoka wiki kadhaa zilizopita na kusema kuwa yupo katika hospitali huko Hurricane Mills na kuwa yupo chini ya uangalizi wa madaktari. Lynn aliweza kutuma sms kupitia watu wake wakaribu na kuwajulisha kuwa anaendelea vizuri katika matibabu yake. Mkali huyo wa muziki wa County aliye na miaka 85 alianza kuonesha matumaini ya kukabiri ugonjwa huo tangu Novemba mwaka jana, lakini hamna taarifa iliyotoka kuwa anaweza kurudi kuendelea na muziki.