MSANII AIKA AFUNGUKA KUHUSU NDOA YAKE NA NAHREEL

Bofya Hapa

                     BAADA ya tetesi kuzagaa kuwa mwanadada Aika Mariale na mpenzi wake wa siku nyingi, Nahreel, wanaounda kundi la muziki wa kizazi kipya la Navy Kenzo, wapo kwenye mipango ya ndoa, mwanadada huyo amefunguka kuwa hakuna kitu kama hicho kwa sasa.

 

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Aika wa nahreel alisema watu wanapenda kuzusha mambo wasiyoyajua na suala hilo halipo kabisa wala hakuna anayewaza kitu hicho kwa sasa zaidi ya kufikiria jinsi ya kuandaa kazi nzuri za kuwakata kiu mashabiki wao.

 

Suala la mimi kuolewa watu watasubiri sana maana hata mipango hiyo haipo kabisa nashindwa hata kulizungumzia, ndoa yetu si leo wala kesho kama ikifika wakati mambo yakiwa tayari tutaweka wazi ila ni huko baadaye sana,” alisema Aika.