Mti wa ajabu wang’olewa Mwanza

Bofya Hapa

Wakazi wa jiji la Mwanza hususani wanaotumia barabara ya Pasiansi wameweza kufanikiwa kung’oa mti uliokuwa ukisumbua kwa kuwa na imani za kishirikina. Mti huo aina ya mwembe uliokuwa ukitoa sauti za binadamu ukipinga using’olewa, uliweza kung’olewa siku ya jana baada ya kusumbua kwa muda mrefu, Zoezi la kuung’oa mti huo ulianza tangu siku ya jumamosi na kisha kushindikana kumalizika ndipo kibarua kikaendelea hapo jana na hatimaye usiku likakakmilika. Shughuli za kuutoa mti huo ili kupisha utanuzi wa barabara katika eneo la Pasiasi kuelekea Uwanja wa ndege wa Mwanza ulivuta hisia za watu wengi tangu jumamosi na hadi jana usiku wakazi wa eneo walikuwepo katika kusaidia kuutoa mti huo wa maajabu.