MWAKA 2018 NI MOTO,THEA NAYE AJA NA LAKE,AFUNGUKA

Bofya Hapa

STAA wa Filamu za Kibongo, Salome Urassa ‘Thea’ ameweka wazi kuwa, baada ya kutengana na mumewe Mike Sangu na kukaa kimya muda mrefu, sasa anatangaza rasmi kwamba mwaka huu ndio mwaka wake wa kuingia kwenye ndoa nyingine iwapo Mungu atamjalia. Akipiga stori na Risasi Jumamosi Thea alisema kuwa, anavyoona yeye kwa mipango ya Mungu mwaka huu atapata ndoa nyingine kwani ni mwaka wa baraka kwake. “Nitaolewa mwaka huu ni mwaka wa baraka na ninaamini Mungu atanijaalia kama ninavyomuomba, ili mambo na mipango niliyoipanga isiende tofauti,” alisema Thea. STORI: HAMIDA HASSAN