MWANDISHI MMAREKANI AKAMATWA, ADAIWA KUMTUSI RAIS MUGABE

Bofya Hapa
U.S. Citizen Martha O' Donovan appears at the Harare Magistrates court escorted by a plain clothes police officer shielding her face in Harare, Saturday, November, 4, 2017. Police arrested and charged Donavan with subversion for allegedly insulting President Robert Mugabe on Twitter as a "sick man," lawyers said Friday. The offense carries up to 20 years in prison. (AP Photo/Tsvangirayi Mukwazhi)

MWANDISHI wa Marekani, Martha O’Dovovan, hivi majuzi alikamatwa na kufikishwa mahakamani mwanzoni mwa mwezi huu nchini Zimbabwe kwa kosa la kumwita Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo “mchoyo na mtu mgonjwa”.
O’Donovan ambaye aliachiwa kwa dhamana, anakabiliwa na kifungo kisichofikia miaka 20 jela akipatikana na hatia.
Mwandishi huyo ambaye alikana kosa hilo alilodaiwa kuliandika kwenye mtandao wa Twitter, alikabidhi pasipoti yake mahakamani na anatakiwa kuripoti polisi mara mbili kwa wiki wakati kesi yake iliyoahirishwa itakaposikilizwa mahakamani.Mahakamani, mwandishi huyo alisema madai hayo ya kumtukana rais huyo mwenye umri wa miaka 93, hayana msingi na yana lengo la kumchafua.

U.S. Citizen Martha O’ Donovan appears at the Harare Magistrates court escorted by a plain clothes police officer shielding her face in Harare, Saturday, November, 4, 2017. Police arrested and charged Donavan with subversion for allegedly insulting President Robert Mugabe on Twitter as a “sick man,” lawyers said Friday. The offense carries up to 20 years in prison. (AP Photo/Tsvangirayi Mukwazhi)

Kukamatwa kwa mwandishi huyo kunafanyika mara ya kwanza tangu Mugabe ateue rais wa masuala ya mtandao mwezi mmoja uliopita, jambo ambalo lilishutumiwa na wanaharakati kwamba lilikuwa limelengwa kwa vyombo vya habari.O’Donovan amekuwa akifanya kazi na televisheni ya Magamba ya nchini humo ambayo huelezea vipindi vyake kuwa ni vya burudani na kuchekesha.

NA WALUSANGA NDAKI/GPL