NAY WA MITEGO NA SIRI YA KUJILIPUA TENA!

Bofya Hapa

              Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’. MWANAMUZIKI anayefanya vizuri kwenye gemu ya Muziki wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka mambo mengi kuhusu kazi zake za muziki kwa sasa. Akichonga na Showbiz, Nay anayebamba na Ngoma ya Makuzi ameamua kuweka wazi siri ya kujilipua kwa mara nyingine katika upande wa video kwa kutengeneza video inayoonekana kukiuka maadili ya Kitanzania.

 

                          Ameelezea mambo mengi ikiwemo video hiyo, ugomvi na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), tofauti kati yake na R.O.M.A na mengine mengi. Huyu hapa; Showbiz: Unazungumziaje ujio wako mpya, umefi ka mahali ulipokuwa umelenga ama Kiba amekufi cha na Seduce Me yake? Nay: Wimbo wangu umefi ka mbali kuliko hata matazamio yangu. Ukitaka kuthibitisha hilo angalia mitaani namna unavyoimbwa, kwanza ‘Maku’ kwa sasa ndiyo msemo wa mjini.

 

Alikiba. Showbiz: Lakini tumeona nyimbo zilizofanya vizuri ukiwemo Seduce Me, Zimbabwe na Utaniua zinagombea namba YouTube, huoni kama umefi chwa na unaukataa ukweli? Nay: Siku zote mafanikio ya nyimbo zangu siyo kwenye mitandao ya kijamii, ni mtaani, haijalishi YouTube upo vipi, ama unachezwaje kwenye mitandao ya kijamii, ili hali mtaani unakubalika basi unafanya vizuri. Showbiz: Mara kwa mara umekuwa ukijilipua kwa kutoa video ambazo hazina maadili na kupambana na rungu la Basata kwa sasa umejilipua tena, hili unalizungumziaje?

 

Nay: Nimetoa video zenye ‘version’ mbili. Ya kuchezwa redioni na nyingine mtandaoni tu. Kwa hiyo sioni kama kuna tatizo. Halafu kwa nini akifanya Nay watu ndiyo wanazungumza, alitoa A.Y Zigo lakini fresh tu na wasanii wengine wamekuwa wakitoa video za kuchezwa mitandaoni au usiku tu, lakini mimi nikitoa ndiyo kila mmoja anazungumza hilo tu, ifi ke hatua watu waelewe kuwa muziki unaturuhusu kufanya kila kitu ilimradi tusivunje masharti.

 

Showbiz: Unaonekana unamchokonoa Kiba, maana kwenye wimbo wako umemuimba kwamba watu wamechoshwa na stori zake? Nay: Si mchokonoi bali ni kweli. Kuna mambo mengi zaidi ambayo watu wanahitaji kuyasikia. Nay wa Mitego: Unazungumziaje suala la kuwepo na timu kwenye muziki? Showbiz: Naamini zinaleta changamoto kwenye muziki na watu kufi kiria kufanya zaidi ya wanavyofanya katika muda husika. ROMA. Showbiz: Unazungumziaje R.O.M.A kukudis kwenye wimbo wake kwamba wewe siyo Rais wa Manzese maana hata ubunge tu haukufai, mna bifu?

 

Nay: Sina bifu na R.O.M.A na hiyo ni changamoto tu kwenye muziki maana hata mimi huwa ninawaimba wengine. Showbiz: Nani mshindani wako hasa kwenye muziki? Nay: sina mshindani maana mimi na jeshi langu la watu wawili kwenye muziki ambao wanashindana wenyewe. Yaani ukiachana na mimi Emmanuel, kuna Mr Nay na Nay wa Mitego, hawa ndiyo wanashindana kwenye muziki.

 

Showbiz: Fafanua kidogo, Nay wa Mitego ni nani na Mr Nay ni nani? Nay: Nay wa Mitego ni mwanamuziki ambaye yupo tangu zamani. Ndiye anayechana kwenye gemu na kaimba Makuzi na nyimbo nyingi za kuchana, lakini Mr Nay yeye anaimba nyimbo za kuchezeka. Showbiz: Kama Mtanzania unazungumziaje suala la kupigwa risasi kwa mbunge na mwanasheria, Tundu Lissu. Nay: Nimekwishampa pole kama ambavyo yeye alifanya nilipopatwa na matatizo. Mengine siwezi kuyazungumzia aisee yasije kunikuta!