NEYMAR AGEUKA MZEE WA MKWANJA, SASA KUTIMKIA REAL MADRID

Bofya Hapa

STAA wa soka Raia wa Brazil anayekipiga katika Klabu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa, Neymar Jr (25) anahusishwa kutimkia Santiago Bernabeu kunako Klabu ya Real Madrid anayoinoa Mfaransa, Zinadene Zidane kwa ada ya paundi milioni 400. Rais wa Madrid, Florentino Perez amezungumzia kumsajili mshambuliaji huyo aliyejiunga na PSG mwanzoni mwa msimu huu akitokea Barcelona kwa ada ya paundi milioni 222. Neymar tayari amefanya mazungumzo na wakala wake na kumuomba kutimiza dili hilo la kuhamia Real Madrid ambapo amesema anapenda kucheza La Liga, ligi moja na Messi. Perez amesema; “Kuwa ndani ya Madrid hukuwezesha kushinda taji la Ballon d’Or kirahisi. Madrid ni timu inayowawezesha wachezaji wakubwa kupata kila kitu wanachokihitaji, kila mtu anafahamu hilo nahitaji kumsajili. Nina hitaji kuwa na wachezaji bora, hili halina shaka, Neymar ni mmoja wao, Nimemfungulia mlango kama anahitaji kujiunga nasi, namkaribisha sana.” Kwa mara ya kwanza Neymar aliwahi kufanya mazoezi na Madrid akiwa na umri wa miaka 14 wakati nyota wa timu hiyo akiwa Dani Carvajal. Ingawa mchezaji huyo alifanya maamuzi ya kurejea kwao Brazil, mwaka 2013, Real Madrid walimuita Neymar na kufanikiwa kufaulu vipimo vya afya lakini aliamua kutimkia Barcelona. Hii ni mara ya tatu Real Madrid wanajaribu bahati yao ya kumsajili.