OMMY DIMPOZ NAYE KAMA ALI KIBA,SASA MAMBO NI MOTO,WAJA KIVINGINE TENA

Bofya Hapa

Baada ya msanii Alikiba kupost picha zinazo muonesha akiwa na muonekano mpya kichwani kwa kubadilisha rangi ya nywele na kuweka nyekundu, sasa msanii Ommy Dimpozi na yeye amepost picha inayomuonesha akiwa na muonekano tofauti wa nywele kwa kuweka nywele rangi ya brown.

Ommy Dimpozi kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost, post mbili, ya kwanza akiwa yupo na Alikiba na kuandika caption iliyosomeka.Hapa Rangi tu 😂 @officialalikiba” na katika post ya pili Ommy Dimpozi amepost picha akiwa na Alikiba pamoja na Seven Mosha na kuandika caption iliyosomeka Aisee @sevenmosha na wewe si upake rangi ya Blue #HapaRangiTu” – Ommy Dimpozi G