PAPII KOCHA KUWAUNGA MKONO ASLAY NA NANDY ESCAPE ONE

Bofya Hapa

Muimbaji Papii Kocha baada ya kuachia video yake ya wimbo ‘Waambie’ na kukamata trending katika mtandao wa YouTube, ametangaza kuwepo kwenye show ya Nandy na Aslay itakayofanyika Jumamosi hii katika ukumbi wa Escape One jijini Dar es salaam.

Hii ndio itakuwa show yake kubwa muimbaji huyo toka atoke gerezani pamoja na Baba yake kwa msamaha wa Rais John Pombe Magufuli. Akiongea na Clouds FM, PapiiKocha amesema anawashukuru sana Watanzania kwa kuupokea vizuri wimbo wake mpya.

Amesema Jumamosi hii ataweka shukrani zake hadharani kwa mashabiki kwani ameomba kupanda kwenye jukwaa la Aslay Nandy ili kutoa shukrani zake. Papii amesema atatumbuiza katika namna ya kipekee na kuonyesha love kwa wadogo zake Aslay na Nandy.