RAIS MAGUFULI AFICHUA SABABU YA KUCHELEWA KUMTEUA JAJI MKUU

Bofya Hapa

                           Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amefafanua sababu ya kuchukua muda mrefu kumteua Jaji Mkuu. Akiongea wakati wa kumuapisha Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma Ikulu jijini Dar es Salaam Jumatatu hii, Rais Magufuli amesema sababu ya kuchukuwa muda mrefuu kufanya uteuzi huo ni kutaka kujiidhisha kwa mtu ambaye amemteua kukalia kiti hicho.

 

               Na ndio maana nimechukua muda mrefu kuteua Jaji Mkuu, kwanza nilitaka kuteua Jaji Mkuu atakayekaa muda mrefu, sio baada ya miaka miwili nilazimike kuteua tena Jaji Mkuu. Na pili nilitaka nijiridhishe huyu nitakayemteua ataweza kupambana na rushwa?

 

Maana rushwa imetapakaa kila mahali, serikalini kuna rushwa, mahakamani kuna rushwa,” amesema Rais Magufuli. Aidha Rais Magufui ameongeza kuwa hajamteua jaji huyo kwa shinikizo kutoka kwa mtu yoyote. J