Rais Magufuli Mgeni Rasmi Siku ya Sheria Nchini

Bofya Hapa

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya sheria leo jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia tarehe 27 hadi 31,Januari 2018. Kushoto ni Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Hussein Kattanga.

Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma (kulia) kuhusu maadhimisho ya wiki ya sheria leo jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia tarehe 27 hadi 31, Januari 2018. Kushoto ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Catherine Revocati.

Msajili Mkuu wa Mahakama Catherine Revocati akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wao na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma (wapili kutoka kulia) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga na Jaji Kiongozi Ferdinand Wambali.

(Picha na: Frank Shija – MAELEZO