RAIS NKURUNZINZA ATANGAZWA KUWA KIONGOZI WA MAISHA CHAMA TAWALA

Bofya Hapa

Chama tawala nchini Burundi, CNDD/FDD kimemtangaza Rais Pierre Nkurunzinza kuwa kiongozi mkuu wa kudumu wa chama hicho baada ya vikao vya siku tatu vya mkutano mkuu wa chama uliofanyika Buye, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Uamuzi huo ambao CNDD/FDD kimesema ni kwa lengo la kuimarisha chama tawala na taasisi zake, umekuja ikiwa inajiandaa kufanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelelea kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034. Wadadisi wa siasa za Burundi wanaamini kuwa hatua hii ya chama tawala inanuwia kumalizia mjadala wa mrithi wa kiti cha Urais kwa niaba ya Chama hicho na kuonyesha mustakabali wa uongozi kabla hata uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2020.

Pia, uamzi huo unapeleka ujumbe kwa wafuasi wa CNDD/FDD na viongozi wenye nia ya kuwania nafasi hiyo kujiepusha na mpasuko wa chama tawala kama ilivyotokea mwaka wa 2015 katika mzozo kuhusu muhula wa sasa wa Rais Nkurunzinza.